1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Umoja wa Mataifa - UN

Umoja wa Mataifa ni chombo kinachonuwia kuendeleza ushirikiano baina ya mataifa. Shirika hilo lilianzishwa Oktoba 24, 1945 kuchukuwa nafasi ya Shirikisho la Mataifa, lililoshindwa kuzuwia vita kuu vya pili vya dunia.

Wakati wa kuasisiwa kwake, Umoja wa Mataifa ulikuwa na wanachama 51. Hivi sasa una wanachama 193. Makao makuu ya umoja huo yako Manhattan, New York. Ofisi nyingine ziko mjini Geneva, Nairobi na Vienna. Malengo makuu ya Umoja wa Mataifa ni pamoja na kulinda amani na usalama kimataifa, kutetea na kulinda haki za binaadamu, kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii, kulinda mazingira, na kutoa msaada wa kibinaadamu yanapotokea majanga ya asili, njaa na migogoro ya kivita.