1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Nje wa Ujerumani ziarani Indonesia

27 Februari 2008
https://p.dw.com/p/DDvN

JAKARTA:

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier akiwa katika ziara ya siku tano Kusini-Mashariki ya Asia,hii leo anakutana na Rais Susilo Bambang Yudhoyono na Waziri wa Nje Hassan Wirajuda wa Indonesia mjini Jakarta.Vile vile atakutana na Surin Pitsuwan alaie Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola ya Kusini-Mashariki ya Asia-ASEAN.

Mwaka jana,Umoja wa Ulaya na ASEAN zilikubaliana kuwa na ushirikiano wa karibu zaidi katika sekta mbali mbali kama usalama na ulinzi wa mazingira.Kutoka Indonesia,waziri Steinmeier ataelekea Singapore na Vietnam.