1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Liberata Mulamula

Liberata Mulamula Rutageruka ni mwanadiplomasia wa Tanzania na mwanasiasa anaehudumu kwa sasa katika wadhifa wa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki tangu Aprili 2021.

Balozi Mulamula ana historia ya zaidi ya miaka 35 kama mwanadiplomasia na mtawala katika wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kikanda, ikiwemo balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa mjini New York, Canada na Marekani. Kabla ya kustafu diplomasia Aprili 2016, alihudumu kama katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje kwa muda wa miezi saba, kati ya Mei 2015 hadi Desemba 2015. Pia alihudumu kama Katibu Mtendaji wa kwanza wa Jumuiya ya Mataifa ya Kanda ya Maziwa Makuu (ICGLR), yenye makao yake Bujumbura, Burundi, kutoka 2006 hadi 2011. Katika wadhifa huo, alisimamia amani, utulivu na maendeleo katika mataifa 11 ya kanda ya Maziwa Makuu.