Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand atathmini kurejea nyumbani | Habari za Ulimwengu | DW | 24.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand atathmini kurejea nyumbani

BANGKOK:

Vyama vya kisiasa nchini Thailand vimeanza mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto.

Washirika wa waziri mkuu alieondolewa na majeshi-Thaksin Shinawatra wanasema wako na uungaji mkono wa kutosha wa kuunda serikali ,ingawa hawajatangaza washirika wao .

Katika uchaguzi wa wabunge uliofanyika jumapili- chama cha People Power Party-PPP- kimeshinda wingi wa viti lakini chini ya nusu ya viti vyote 480.

Chama cha PPP kimeahidi kumrejesha nyumbani Thankisin ambae sasa yuko uhamishoni. Kuhusu kinachoendelea sasa nchini mwake, waziri mkuu huyo aliepinduliwa na jeshi anapendekezo.

Thanksin amekuwa uhamishoni tangu apinduliwe Septemba mwaka jana.Kwa mda huohuo Washington imekaribisha ripoti za awali zinazoonyesha kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com