1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Martin Schulz

Martin Schulz ni mwanasiasa wa chama Kisoshalisti SPD cha nchini Ujerumani. Alikuwa spika labunge la Ulaya na sasa ndiye mwenyekiti wa chama hicho na mgombea wake wa nafasi ya kansela katika uchaguzi mkuu wa 2017.

Schulz alipamba vichwa vya habari aliposhambuliwa kwa maneno na waziri mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi mwaka 2003, Mbunge wa UK katika bunge la Ulaya Godfrey Bloom mwaka 2010, na wakati alipotoa kauli tata katika hotuba yake mbele ya bunge Israel Knesset mwaka 2014. Schulz anasema anazungumza kwa ufasaha lugha za Kijerumani, Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kitaliana na Kidachi.

Onesha makala zaidi