Waziri Mkuu wa zamani wa Canada akiri kapokea hela lakini asema sio murungura | Habari za Ulimwengu | DW | 14.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Waziri Mkuu wa zamani wa Canada akiri kapokea hela lakini asema sio murungura

Waziri mkuu wa zamani wa Canada, Brian Mulroney, amekanusha madai kuwa alipokea rushwa alipokuwa ofisini mwaka wa 1988.Inadaiwa kuwa murungura aliula kutoka kwa mfanya biashara ya silaha wa Ujerumani. Lakini akiwa mbele ya kamati ya kibunge mjini Ottawa Canada- amekiri kuchukua dola za Kanda zaidi ya laki mbili kutoka kwa Karlheinz Schreiber baada ya kuondoka ofisini mwaka wa 1993.Mulroney asema hilo lilikuwa kosa.

Mjerumani Schreiber anatakiwa Ujerumani kwa madai kadhaa mkiwemo kukwepa kulipa kodi,ufisadi pamoja na udanganyifu.Waongoza mashataka wa Ujeruamni wanaamini kuwa raia huyo ni mhusika mkuu katika kashfa ya kufadhili chama, ambapo chama cha Christian democtratic Party –CDU- cha Kansela wa zamani wa Ujerumani-Helmut Kohl, kilihusishwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com