Waumini wa kikristo wanasherehekea Pasaka kote ulimwenguni | Habari za Ulimwengu | DW | 08.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Waumini wa kikristo wanasherehekea Pasaka kote ulimwenguni

Vatikan:

Maelfu ya waumini wa kikatoliki wamekusanyika katika uwanja wa Peter mjini Roma,kusherehekea misa ya pasaka pamoja na kiongozi wa kanisa katoliki Benedikt wa 16.Misa hiyo ndio kilele cha siku kuu ya Pasaka.Kiongozi wa kanisa katoliki anatazamiwa kama kawaida kuubariki Mji na ulimwengu-Urbi et Orbi.Jana usiku kiongozi wa kanisa katoliki Benedikt wa 16 alikesha katika uwanja wa Peter kwa ibada ya pasaka pamoja na waumini wa kutoka sehemu mbali mbali za dunia.Aliwasha moto wa pasaka-kitambulisho cha kufufuka Nabii Issa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com