Watu wasiopungua wanne wameuwawa katika mripuko wa bomu | Habari za Ulimwengu | DW | 05.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Watu wasiopungua wanne wameuwawa katika mripuko wa bomu

-

SANAA

Zaidi ya watu wanne wameuwawa katika mripuko wa bomu uliotokea karibu na afisi ya posta kaskazini mwa mkoa wa Saada nchini Yemen. Maafisa wa serikali katika eneo hilo wanasema shambulio hilo limefanywa na mshambuliaji wa kujitoa muhanga kutoka kundi la vijana waasi wa kishia ambalo linapambana dhidi ya jeshi katika eneo hilo la Saada tangu mwaka 2004.

Shambulio hilo ni la pili kutokea katika kipindi cha miezi miwili.Saada ni eneo la milimani linalopakana na Saudi Arabia kiasi kilomita 230 kutoka kaskazini mwa mji mkuu wa Yemen Sanaa na huko ndiko wanakokutikana kundi hilo la vijana wakishia linalojiita Houthis ambalo linaendesha vita dhidi ya wanajeshi wa serikali.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com