Watu wanane wauwawa katika shambulio la bomu Mogadishu | Habari za Ulimwengu | DW | 03.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Watu wanane wauwawa katika shambulio la bomu Mogadishu

Raia takriban wanane wa Somalia, wengi wao wakiwa wanawake, wameuwawa leo wakati basi walimokuwa wakisafiria lilipolipuliwa na bomu la kutegwa ardhini katika mji mkuu wa Somali, Mogadishu.

Kwa mujibu wa walioshuhudia, watu wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mlipuko huo uliotokea katika barabara ya Afisiyone kusini mwa Mogadishu.

Dereva wa basi hilo, Abdulahi Moalim, amenusurika na amesena maiti za abiria waliouwawa ziko katika hali mbaya huku baadhi zikiwa zimechomeka kiasi cha kutoweza kutambulika.

Wakaazi wanasema basi hilo lilikuwa likielekea katika kitongoji cha Hamarweyne mjini Mogadishu likiwa limewabeba wanawake wanaouza miraa wakati shambulio hilo lilipotokea. Polisi wamelifunga eneo hilo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com