1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Sergei Skripal

Sergei Viktorovich Skripal ni afisa wa zamani wa intelijensia katika jeshi la Urusi aliekuwa akiitumikia pia idara ya ujasusi ya Uingereza katika miaka ya 1990 na mwanzoni mwa 2000.

Skripal alikamatwa Desemba 2004 na idara ya usalama ya Urusi FSB na baadae alishtakiwa na kutiwa hatiani kwa uhaini wa hali ya juu, ambapo alihukumiwa kifungo cha miaka 13 gerezani. Alihamia nchini Uingereza mwaka 2010, kufuatia programu ya kubadilishana wahalifu wa ujasusi. Machi 4, 2018 Skripal na binti yake Yulia aliemtembelea kutoka Moscow, walishambuliwa kwa sumu aina ya Novichok katika mji wa Salisbury nchini Uingereza. Shambulizi hili lilizusha mgogoro mkubwa kati ya Uingereza na washirika wake wa Magharibi kwa upande mmoja, na Urusi kwa upande wa pili, ambayo walliituhumu kwa kuhusika na shambulio hilo. Urusi inakanusha.