Wataliban wamemuachia huru mtumishi wa Terre d′Enfance | Habari za Ulimwengu | DW | 12.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Wataliban wamemuachia huru mtumishi wa Terre d'Enfance

Paris

Mtumishi wa shirika la misaada ya kiutu la Ufaransa,-Terre d’Enfance-Eric DAMFREVILLE aliyeachiwa huru baada ya kutekwa nyara kwa muda wa siku 38 amerejea nyumbani nchini Ufaransa hii leo.ERIC DAMFREVILLE alikua akishikiliwa pamoja na mwentake wa kike na wakalimani wao watatu wa kiafghanistan tangu April tatu iliyopita.Wataliban walimuachia huru mfanyakazi mwenzake wa kike April 28 iliyopita.Hatima ya waafghani watatu haijulikani.Serikali ya Ufaransa imesema itaendelea kupigania na wao pia waachiliwe huru.Eric DAMFREVILLE aliepelekwa katika hospitali ya kijeshi mjini Paris kwa matibabu,amesema waliomteka nyara hawakumsumbua.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com