Wasifu wa Vladimir Putin | Matukio ya Kisiasa | DW | 28.02.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Wasifu wa Vladimir Putin

Putin anasema amefanikiwa katika kipindi chake cha uongozi akiwa Rais wa Urusi.

default

Kiongozi wa Urusi Vladimir Putin.

Vladimir Putin atamaliza muda wake kama kiongozi wa taifa hilo la Urusi baada ya uchaguzi wa rais tarehe 2 Machi mwaka huu. Binafsi amezungumzia juu ya mafanikio ya kipindi chake uongozi. Akiizungumza katika mkutano na waandishi habari ikulu mjini Mosko hivi karibuni wakishiriki zaidi ya waandishi habari 1300 wa ndani na kutoka nchi za nje, Putin alisema kwa miaka mingi alitumika usiku na mchana

Putin aliingia madarakani Desemba 1999 baada ya kujiuzulu mtangulizi wake Boris Yeltsin na kumpendekeza Putin kuwa mgombea wa wadhifa wa Rais. Mwezi Machi 2000 Putin akashinda uchaguzi wa rais kwa 52.9 asili mia. Baada ya miaka kadhaa kashfa za kisiasa na matatizo ya kiuchumi, kuingia madarakani Putin kukazusha matumaini ya kua na mwanzo mpya na utulivu.

Kipindi cha kwanza cha madaraka yake kilikua cha kuleta mageuzi katika siasa ya ndani- nchi za magharibi zinawa na shaka shaka upande huo. Mageuzi yake yakawa ni kuhakikisha utendaji na uwajibikaji katika ngazi za uongozi hadi upande wa magavana wa mikoa. Akawaandama matajiri waliokua wameikumbatia ikulu , akisaidiwa na vyombo vya habari. Miongoni mwao ni Boris Beresowski aliyekimbilia uhamishoni na sasa anaishi Uingerreza.

Moja kati ya changa moto zilizomkabili katika kipindi chake cha kwanza ni ile ajali ya nyambizi" Kursk" ilioazama Agosti 2000 na mabaharia 23 kupoteza maisha yao. Hakuna aliyeweza kunusurika katika ajali hiyo Tukio hilo lilizusaha mkasa mkubwa kwani wakati huo Putin alikua likizoni Sotschi na kuchelewa kurudi Mosko kukazusha malalamiko makali kutoka kwa jamaa za waliouwawa.

Suala kubwa na zito kwa Putin ulikua mzozo wa Chechnya.Kwa kutumia hoja ya ugaidi akachukua msimamo mkali kupambana na wapiganaji wa Chechnya.

Oktoba 2002 magaidi wakichechnya wakalivamia jumba la michezo ya kuigiza mjini Mosko na kuwashikilia mateka watu karibu mia moja. Putin akachukua msimamo mkali kukabiliana nao akiamuru wanajeshi kulivamia jengo hilo. Hatua hiyo ikasababisha kuuwa sio tu kwa baadhi ya mateka bali pia magaidi wote. Huo ukawa mwanzo wa hatua za Putin kuhakikisha anaumaliza mgogoro wa Chechnya kwa nguvu za kijeshi.

Machi 2004, Putin akapata ridhaa nyengine ya wapiga kura akichaguliwa kwa wingi wa 70 asili mia ya kura. Katika mhula wake wa pili, akaamua kuishughulikia sera ya kigeni na kurudisha tena Urusi katika jukwaa la kimataifa. Msimamo wa Urusi ukakosolewa na Marekani na nchi za magharibi. Putin akaanza kuviandama vyombo vya habari na waandishi wa habari wenye kuukosoa utawala wake.

Oktoba 2006 mwandishi habari Anna Politkovskaya,mkosoaji mmoja wapo mkubwa wa utawala wa Putin ikiwa ni pamoja na kukanmamizwa kwa demokrasia nchini humo, aliuawa kwa kupigwa risasi nje ya nyumba yake mjini Mosko.

Moja wapo ya mafanikio ya Putin ni utulivu wa uchumi na ukuaji wa uchumi wa Urusi pamoja na kuboreka kwa nafasi za uwekezaji. Pia Urusi ni mshirika wa kiuchumi hasa kutokana na utajiri wake wa nishati- mafuta na gesi. Lakini mali ya asili inatumiwa pia na Putin kama silaha ya kushinikiza matakwa yake kwa majirani wasioonekana kufuata maelekezo ya Kremlin.

Katika mgogoro mmoja wapo na Ukraine kwa kile kilichoonekana kuelemea upande wa magharibi, Urusi ikatishia kukata usambazaji mafuta kwa Jamhuri hiyo. Akizungumzia mafanikio yake akasema," Ninashangazwa binafsi kwamba sasa Urusi imeanza kupiga hatua kubwa ya maendeleo. Ni hatua ya utulivu na ukuaji uchumi na kwa msingi huo kuyatatua matatizo ya kimaii kazi muhimu upande huo ni kupunguza pengo kati ya wale wanaoishi vyema nchini Urusi na wenye utajiri mkubwa na wale ambao bado wanatapia maisha. Pengo hili tunapaswa na ni lazima kuliondoa."

Baada ya kuacha Urais Putin anatarajiwa kugawana madaraka na rais mtarajiwa Medvedjev ambaye ni chaguo lake, huku Putin akiwa Waziri mkuu.Vladimir Vladimirovich Putin mwenye anasema"mtu hapaswi kusikitika kwamba anaacha wadhifa fulani bali anapaswa kufurahi kwamba atakua na wadhifa kuweza kuwajibika zaidi."

 • Tarehe 28.02.2008
 • Mwandishi Rabitz,Cornelia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DE69
 • Tarehe 28.02.2008
 • Mwandishi Rabitz,Cornelia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DE69
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com