WASHINGTON:Wolfowitz asema ni mhasiriwa wa njama za kumpaka Tope | Habari za Ulimwengu | DW | 01.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Wolfowitz asema ni mhasiriwa wa njama za kumpaka Tope

Rais wa benki kuu ya dunia Paul Wolfowitz anadai amekuwa mhasiriwa wa kampeini ya kumpaka matope inayolenggwa kumlazimisha ajiuzulu wadhifa wake.

Wolfowitz hata hivyo amesema hatojiuzulu kutokana na madai ya kashfa yanayomuandama ambayo ameyataja kuwa hayana maana.

Ameyasema hayo mbele ya jopo linalosikiliza malalamiko yake kuhusiana na kile kinachosemwa kwamba alimpandisha cheo na kumuongeza mshahara mpenzi wake wa kike Shaha Riza.

Kamati hiyo inachunguza pia hatua ya bwana Wolfowitz ya kuwaajiri wasaidizi wa zamani wa ikulu ya White House katika nyadhifa muhimu na zenye mshahara mnono.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com