1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

JINSIA & MWILI

Kwa kiasi kikubwa jamii bado inaona aibu kuzungumza kwa uwazi masuala yahusuyo uzazi. Bado kuna usiri mkubwa kati ya mzazi na mwanae ama hata wenza kuzungumzia viungo vya uzazi ambavyo wengi huviita "Sehemu za siri".

Mabadiliko yaliyopo sasa yanaathiri kwa namna moja ama nyingine tamaduni, mila na hata desturi zetu. Lakini je, huwa tunafikiria madhara kama mimba za utotoni ama maradhi iwapo tutaendelea kukumbatia mila zetu? Kwenye makala za Jinsia na Mwili tunazungumzia kwa uwazi na kina sehemu zile za siri, lengo likiwa ni kuikumbusha jamii kwamba hivi ni viungo vya kawaida tu vya mwili na hakuna sababu ya kuona aibu kuvizungumzia.