1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Rodrigo Duterte

Rodrigo "Rody" Roa Duterte, maarufu pia kama Digong, ni mwanasheria na mwanasiasa wa Ufilipino ambaye ni rais wa 16 na wa sasa wa Ufilipino tangu Juni 2016. Ndiye mkaazi wa kwanza kutoka Mindanao kushika wadhifa wa rais.

Mei 9 2016, Durtete alishinda uchaguzi wa rais kwa asilimia 39.01 ya kura, katika uchaguzi uliowashirkisha wagombea wengine wanne. Wakati wa kampeni yake, aliahidi kupuguza uhalifu kwa kuwauwa maelfu ya wahalifu. Sera yake ya ndani imejikita katika kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya kwa kuanzisha vita vya Ufilipino dhidi ya madawa ya kulevya. Kwa mujibu wa polisi ya taifa ya Ufilipino, idadi ya vifo ilipindukia 7,000 kufikia Januari 2017, na baada ya hapo polisi ilisitisha utoaji wa taarifa za waliouawa. Baada ya ukosoaji wa watalaamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, alitishia kuiondoa Ufilipino katika umoja huo na kuunda shirika jipya pamoja na China na mataifa ya Afrika. Katika ukurasa huu utapata maudhui za DW kuhusu Durtete.

Onesha makala zaidi