Ufilipino yawakamata raia wake wanaoifanyia ujasusi China
4 Machi 2026
Ufilipino inasema hatua hiyo inaonesha wazi haja ya uwepo wa sheria kali dhidi ya upelelezi na mataifa ya kigeni kuingilia masuala ya nchi hiyo.
Mamlaka hazikutoa taarifa kuhusiana na kisa hicho, ikiwemo ni watu wangapi wlaiokamatwa au iwapo wamefunguliwa mashtaka.
"Shughuli za watu hawa wanaozifanyia shirika la ujasusila China zimesitishwa," imesema taarifa ya Baraza la Usalama la Kitaifa la Ufilipino.
"Hatua stahiki dhidi ya wahusika ambao wote ni raia wa Ufilipino, zimechukuliwa. Wote wamekiri kuifanyia China ujasusi na wanashirikiana na mamlaka," iliongeza taarifa hiyo.
Uhusiano kati ya China na ufilipino umezidi kuwa mbaya kutokana na makabiliano ya mara kwa mara katika Bahari ya Kusini mwa China, huku pande zote mbili zikizidisha vita vyao vya maneno ambavyo vimejitokeza pia katika miotandao ya kijamii.