1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yalani kudhulumiwa Wapalestina

17 Machi 2026

Ofisi ya haki za binadamu ya UN imesema ina wasiwasi kuhusu uwezekano wa kile ilichokiita takasatakasa ya kikabila dhidi ya Wapalestina.

https://p.dw.com/p/5AYtD
Israel imekuwa ikichukuwa kwa nguvu ardhi ya Wapalestina katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi
Israel imekuwa ikichukuwa kwa nguvu ardhi ya Wapalestina katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi Picha: Ronen Zvulun/REUTERS

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu , imelaani hatua ya Israel ya kutanuwa makaazi ya walowezi na kuwaondosha kwenye ardhi yao maelfu ya Wapalestina katika sehemu kubwa ya Ukingo wa Magharibi, katika miezi ya hivi karibuni.

Ofisi hiyo imesema ina wasiwasi kuhusu uwezekano wa kile ilichokiita takasatakasa ya kikabila dhidi ya Wapalestina.Mataifa ya Kiislamu yalaani udhibiti wa Ukingo wa Magharibi

Ripoti hiyo mpya ya ofisi ya haki za binadamu  inayoendeshwa na Volker Turk  imetazama hali ilivyokuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwishoni mwa mwezi  Oktoba na kutahadharisha juu ya kutanuliwa makazi hayo ya walowezi na kuondolewa kwa nguvu  kwa zaidi ya Wapalestina 36,000.