WASHINGTON:Rais Bush asihi Marekani kukubali sera zake za Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 24.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Rais Bush asihi Marekani kukubali sera zake za Iraq

Rais George Bush wa Marekani amehutubia Bunge la Congress linalosimamiwa na chama cha Demokratik.Hotuba yake inatoa mwelekeo wa taifa.Katika hotuba hiyo Rais Bush anatoa wito kwa Bunge la Congress kufikiria upya sera zake za nchi ya Iraq ambazo zinazua utata vilevile maswala ya utoaji wa huduma za afya na upunguzaji wa matumizi ya gesi nchini humo kwa asilimia 20 katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

.Kulingana na kiongozi huyo kushindwa kwa taifa hilo huenda kukasababisha ueneaji wa ghasia katika eneo zima la Mashariki ya Kati.Rais Bush anapendekeza baraza la viongozi lililo na pande mbili katika Bunge la Congress ili kutathmini hali nzima ya nchi ya Iraq vilevile vita dhidi ya ugaidi.

Kulingana na utafiti thuluthi mbili ya raia wa Marekani wanapinga uamuzi wa Rais Bush wa kupeleka majeshi alfu 20 zaidi nchini Iraq wakati ghasia zinazidi.Wanachama wa Demokratik kwa upande wao walikuwa na mtizamo tofauti.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com