WASHINGTON:Marekani yamkamata kamanda wa Al Qaida | Habari za Ulimwengu | DW | 28.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Marekani yamkamata kamanda wa Al Qaida

Marekani imesema kuwa imemkamata afisa wa ngazi ya juu wa kundi la Al Qaida, ambaye alikuwa akipanga mipango ya kumuua rais wa Pakistan Pervez Musharraf.

Afisa huyo, Abd al Hadi al Iraq alikamatwa alipokuwa akirejea kwao nchini Iraq anakotuhumiwa pia kupanga mashambulizi mapya dhidi ya nchi za magharibi.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani amesema kuwa Abd al Hadi kwa sasa amepelekwa katika jela ya Guantanamo Bay na kwamba ni miongoni mwa watu waliyokuwa wakiaminiwa na Osama Bin Laden.

Nchini Saudi Arabia serikali ya nchi hiyo imesema kuwa imewakamata watu zaidi ya 170 wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Al Qaida.

Msemaji wa Wizara ya mambo ya Ndani ya Saudi Arabia, amesema kuwa watu hao ambao ni kutoka nje na ndani ya nchi hiyo, walikamatwa katika msako mkali dhidi ya magaidi.

Katika msako huo pia polisi walikamata idadi kubwa ya silaha, pamoja na pesa na nyaraka mbalimbali.

Msemaji huyo amesema kuwa baadhi ya wanamgambo hao waliyokamatwa walipata mafunzo nje ya nchi hiyo ya kurusha ndege katika visima vya mafuta nchini Saudi Arabia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com