Washington: Mahakama kuu ya Marekani yakubali kusikiliza kesi za Guantanamo, | Habari za Ulimwengu | DW | 30.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Washington: Mahakama kuu ya Marekani yakubali kusikiliza kesi za Guantanamo,

Mahakama Kuu ya Marekani imekubali kusikiliza kesi endapo washukiwa wa ugaidi wanaozuiliwa Guantanamo wana haki ya kuwasilishwa mbele ya mahakama ya shirikisho kupinga hatua yao ya kuzuiliwa bila kushtakiwa katika gereza hilo lililoko Cuba.

Mwezi Aprili mahakama hiyo ilikataa kusikiliza kesi hiyo wala haijatoa sababu za kukubali kuisikiliza kesi hiyo mara hii.

Uamuzi huo ni pigo kwa serikali ya Rais George Bush ambayo inataka kesi hizo zishughulikiwe na mahakama ya kijeshi pekee.

Kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa mahakamani baadaye mwaka huu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com