1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapi wahamishiwe wafungwa wa Guantanamo ?

27 Januari 2009

Je, Bw.Steinmeier asaka jukwaa la kamepni ?

https://p.dw.com/p/Gh3P
Frank-Walter SteinmeierPicha: AP

Badisches Tagblatt linajishughulisha na hukumu aliopitishiwa mkuu wa zamani wa Shirika la Posta la Ujerumani, Klaus Zumwinkel lkiandika:

"Mwishoe,Bw.Klaus Zumwinkel kama ilivyotarajiwa, ametoka mahkamani huru.

Amepewa kifungo cha nje na faini ya kima sawa na kile ambacho alikwepa kulipa kama kodi.kigogo hicho imara cha zamani cha Posta,alitendewa kana kwamba ni mhalifu wa kawaida asielipa kodi.Na hukumu aliopewa imestahiki ukiilinganisha na kesi sawsa na yake.Kwani, Zumwinkel aliungama madhambi yake na alionesha majuto yake mbele ya mahkama kwa aliotenda."

Gazeti la Nurembergher Zeitung linatuchukua katika mada ya kufungwa kwa gereza la Guantanamo na wapi kuwahamishia wafungwa wake.Laandika:

"Marekani bado haikutoa ombi kwa Ujerumani kuwachukua wafungwa .Lakini ombi likitoka,Ujerumani kwa sababu mbili isilikatae:Kwanza rais Obama anataka kufuta doa na aibu ya gereza hilo na kwa msaada huo huenda nae siku moja akalipa jaza.Pili, je,kweli kuna anaeamini kwa dhati kuwa watu hawa walioathiriwa mno na kifungo cha miaka mingi gerezani......wataweza kuhatarisha usalama wetu ?"

Nord bayerischer Kurier, linasema hata pakiwa hakuna tatizo,mimi huzua tatizo.Ni kwa usemi huo, waziri wa nje wa Ujerumani Bw.Frank -Walter Steinmeier amechochea mjadala iwapo Ujerumani wafungwa wa Guantanamo iwachukue.Gazeti lauliza:

"Je, Bw.Steinmeier anasaka hapo jukwaa la kujipigia debe kwa kampeni ya kuja kuwa kanzela wa Ujerumani ?Asubiri nafasi nyengine bora kwani, Guantanamo si jukwaa linalofaa kwa kampeni ya uchaguzi."