Wapalestina 7 wauawa Ukanda wa Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 06.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Wapalestina 7 wauawa Ukanda wa Gaza

GAZA:

Shambulizi la jeshi la anga la Israel limeua si chini ya Wapalestina 7 na kujeruhi 4 wengine.Shambulizi hilo lililenga kituo cha polisi cha Hamas katika Ukanda wa Gaza.Kwa mujibu wa maafisa wa hospitali mjini Gaza,wote waliouawa walikuwa wanachama wa Hamas,kundi linalodhibiti eneo la Gaza.Msemaji wa majeshi ya Israel amethibitisha shambulizi hilo na kusema kuwa limejibu mashambulizi ya makombora yaliyofanywa kutoka Gaza hapo awali na wanamgambo wa Kipalestina dhidi ya mji wa Sderot kwenye mpaka wa Israel.

Wakati huo huo,chama cha Hamas kimedai kuwa ndio kilichohusika na shambulizi la kujitolea muhanga lililofanywa mji wa Dimona,kusini mwa Israel.Shambulizi hilo liliua mwanamke mmoja wa Kiisraeli na wengine 11 walijeruhiwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com