Wanaanga wa China wafika mwezini | Masuala ya Jamii | DW | 26.09.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Wanaanga wa China wafika mwezini

Chombo cha anga za juu kikiwa katika safari yake ya tatu, leo hii kimefanikiwa kufika mwisho wa safari yake ambayo ni mwezini na mmoja wa wanasayansi watatu waliyoko katika chombo hicho anajiandaa kutoka kuanza kutembea.

Rais wa China Hu Jintao

Rais wa China Hu Jintao

Chombo hicho kilianza safari yake ya kwenda mwezini hapo jana kikiwa na wanaanga watatu, ambao wanatarajiwa kukaa huko kwa muda wa takriban siku tatu, kabla ya kurudi duniani.


Kwa mara ya kwanza mwanaanga huyo ataanza kutembea mwezini kesho Jumamosi saa 2.30 asubuhi kwa saa za Afrika ya Mashariki.


Msemaji wa Shirika la Safari za Anga la China, Wang Zhaoyao aliwaambia waandishi wa habari hii leo ya kwamba chombo hicho kiitwacho Shenzhou 7 yaani chombo kitakatifu cha 7 kimefika salama mwezini na wanaanga hao wanasubiri muda wao uliyopangwa kabla ya kiongozi wao kutoka na kuanza kutembea mwezini.


Kiongozi huyo Zhai Zhigang mwenye umri wa miaka 41 ambaye wakati walipoanza safari hiyo hapo jana alisema kuwa watakabiliwa na changamoto kubwa,atakuwa mchina wa kwanza kutembea mwezini.


Mmoja wa watalaam wa ngazi wa shirika hilo la safari za anga za juu la China Zhang Jianqi amesema kuwa kwa mwananga huyo kutembea mwezini na wenzake wawili kubakia chomboni, ni jaribio kubwa lenye changamoto nzito.


Amesema kuwa mwendo wa kasi wa chombo hicho unaweza kuwasababishia kizunguzungu, kichefuchefu,kutapika pamoja na maumivu makali.Pia wanaweza kupoteza fahamu na kupata matatizo ya kupumua.Hatua hiyo ya China kupelekwa wanaanga mwezini imekuja siku chache tu kabla ya Shirika la Safari za Anga za Juu la Marekani NASA kuadhimisha miaka 50 toka kuanzishwa kwake hapo Oktoba mosi.


Hiyo ni ishara ya kwamba China inaelekea kuwa miongoni mwa mataifa yenye nguvu katika tafiti za anga za juu.


Shirika la Habari la China limetangaza leo ya kwamba hatua inayofuatia ni kurushwa kwa chombo kingine ambacho kitakwenda katika sayari ya Mars.


Aidha China imesema kuwa huenda ikajenga kituo chake cha utafiti angani katika muongo mmoja ujayo.


Japan imeipongeza China kwa hatua hiyo kubwa kisayansi, na kudokeza ya kwanza nchi hizo mbili huenda zikashirikiana siku za usoni katika tafiti za anga za juu.


Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri la Japan Takeo Kawamura amesema kuwa wanafikia hatua ya kuwa na fikra za kushirikiana na China katika sekta hiyo, na kuelezea matumaini yake kuwa mpango huo wa China wa kupeleka chombo anga za juu utatimiza mchango wa China kama taifa lenye amani.


Japan mara kadhaa imekuwa ikielezea wasi wasi wake juu ya kuongezeka kwa harakati za China kuimarisha uwezo wake kijeshi.
 • Tarehe 26.09.2008
 • Mwandishi Liongo, Aboubakary Jumaa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FPSB
 • Tarehe 26.09.2008
 • Mwandishi Liongo, Aboubakary Jumaa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FPSB
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com