Wakuu wa vyama vyote vya kisiasa nchini Irak watoa mwito makundi ya wanamgambo yapokonywe silaha
6 Aprili 2008Mosul:
Wanafunzi 42 waliotekwa nyara karibu na mji wa kaskazini wa Irak-Mosul wameachiwa huru.Vikosi vya usalama vya Irak vimewaokoa wanafunzi hao muda mfupi baada ya kutekwa nyara.Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Irak,watu waliokua na silaha waliyasimamisha mabasi mawili yaliyokua na wanafunzi wa chuo kikuu cha Mosul na kuwateka nyara.Wakati huo huo wakuu wa vyama vyote vya kisiasa vya Irak wamekutana mjini Baghdad hii leo na kuyatolea mwito makundi yote yawapokonye silaha wanamgambo wao na wayavunje makundi hayo.Hilo ndilo sharti pekee la kuweza kuchangia katika utaratibu wa kisiasa na kuishiriki katika uchaguzi ujao nchini humo.Waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na rais Jalal Talabani ,waziri mkuu Nuri El Maliki na wakuu wa vyama vyote vinavyowakilishwa bungeni..