1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Utalii

Matembezi ya kuzunguka dunia kwa sababu za starehe, mapumziko au biashara yanazidi kukua. Ni suala muhimu kiuchumi.

Mwaka 2015 mataifa ya Ulaya yalishika nafasi tatu kati ya tano za juu zilizotembelewa zaidi duniani. Ujerumani ndiyo ina watalii wengi wanaotemebelea sehemu mbalimbali duniani, ambapo Wajerumani hutumia kiasi cha Euro bilioni 80, sawa na dola za Marekani bilioni 89 kila mwaka kutembelea maeneo mbalimbali ya dunia (Marekani inashika nafasi ya pili), licha ya ukweli kwamba Ujerumani inashika nafasi ya nne duniani kwa ukubwa wa pato jumla ya ndani (GDP) na ya 14 kwa idadi ya wakaazi. Ujerumani pia inashika nafasi ya nane kwa idadi kubwa ya watalii wanaoitembelea, ikiingiza kiasi cha Euro bilioni 24 kwa mwaka kutokana na utalii.

Onesha makala zaidi