1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mombasa kivutio cha watalii Afrika Mashariki

23 Agosti 2023

Mombasa inaendelea kuwa kivutio kikuu cha watalii kutoka Afrika Mashariki kwa kasi sana, hasa watalii kutoka Entebbe nchini Uganda. Hii ni kutokana na kuimarishwa kwa biashara kati ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4VUIG
Ufukwe wa Mombasa
Mtalii kutoka Ujerumani akiwa na mume wake MkenyaPicha: picture alliance/dpa

Siku za hivi karibuni watalii kutoka nchi mbalimbali za afrika mashariki kama Uganda na Tanzania wamekuwa wakifurika mjini Mombasa nchini Kenya kuzuru maeneo mbalimbali yanayowavutia watalii.

Hoteli nyingi zilizoko pwani ya mombasa huwa na mandhari ya kupendeza na mzuri wa utulivu wa Bahari ya Hindi.

Mombasa imeanza kuwa kivutio cha watalii wengi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, hasa kutoka Entebbe Uganda kutokana na kuimarishwa kwa biashara kati ya nchi ya Kenya na nchi ya Uganda.

Mombasa Kenya
Mamia ya watu wakifurahia sikukuu ya Christmas fukwe za Mombasa.Picha: Gideon Maundu/AP Photo/picture alliance

Shirika la ndege la Uganda sasa limeutaja mji wa Mombasa kama njia yake kubwa ambayo inawaletea faida. Kwa sasa wana mpango wa kuongeza maeneo ya usafiri wa ndege zao katika pwani ya Kenya. 

Kulingana na Meneja wa kampuni ya ndege za nchini Uganda Peggy Macharia, ndege kutoka nchini Uganda zitakuwa zinawasafirisha watalii hadi mjini Malindi, Ukunda na pia Lamu.

Macharia ameeleza kuwa, kutoka Entebbe ndege hiyo inasafiri katika nchi nyingine 11 za Afrika zikiwemo Tanzania, Burundi, Sudan Kusini, na Afrika Kusini. vilevile Wanatazamia kuanza ndege zao kusafiri hadi Nigeria baada ya miezi mitatu.Ndege hiyo huingia Mombasa kutoka Entebbe, Uganda mara tatu kwa wiki, kwa kutumia ndege aina ya CRJ-900 ambazo hubeba abiria 76.

FE: Kultur 21/24.102.2021 The Wabulushi Community of Mombasa - MP3-Stereo

Mwakilishi wa maendeleo ya soko wa Bodi ya Utalii ya Uganda katika soko la Afrika, Anthony Ochieng ameeleza kuwa, baadhi ya mambo ambavyo yamekuwa yakiwavutia watalii wengi kutoka jumuiya ya afrika mashariki wanaokuja pwani ya Kenya ni matukio, burudani, wanyamapori na michezo ya baharini.

Historia ya mji wa Mombasa na jukumu lake la kuanza biashara ya Afrika Mashariki inayovuka hadi bara imechangia pakubwa kuufanya mji wa Mombasa kuwa maarufu na chaguo la kwanza kwa wasafiri wengi wa afrika mashariki.