1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Yoweri Museveni

Yoweri Kaguta Museveni ni mwanasiasa wa Uganda ambaye amekuwa rais tangu Januari 29, 1986. Museveni alishiriki katika uasi uliyowaondoa madarakani marais wa Uganda, Iddi Amin Dada na Milton Obote.

Katikati mwa miaka ya 1990, Museveni alikuwa akisifiwa na mataifa ya magharibi kama sehemu ya kizazi kipya cha viongozi wa Afrika. Uongozi wake lakini umeshudia ushiriki wa Uganda katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya Jamhuri ya Kidemorasi ya Congo na katika migogoro mingine katika kanda hiyo. ni mmoja wa viongozi waliodumu kwa muda mrefu zaidi barani Afrika na alitangazwa pia mshindi wa uchaguzi mkuu uliyofanyika Februari 18, 2016 - ushindi ambao hata hivyo mpinzani wake mkuu Kizza Besigye alikata kuutambua. Ni Mshirika muhimu wa mataifa ya magharibi na hasa Marekani, katika suala zima la usalama. Ukosoaji umekuwa ukiongezeka dhidi ya utawala wa Museveni, akidaiwa kutumia vikosi vya usalama kusalia madarakani na kukandamiza upinzani.

Onesha makala zaidi