1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Rais Museveni amteua mtoto wake kuwa kamanda mkuu wa jeshi

22 Machi 2024

Rais Museveni amemteua mtoto wake wa kiume Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa kamanda mkuu wa jeshi, uteuzi huo hata hivyo umezua minong'ono huku wengi wakiamini kuwa Museveni anamsafishia njia mtoto huyo kuwa rais.

https://p.dw.com/p/4e04O
Muhoozi Kainerugaba (katikati) akivalishwa cheo kipya cha Luteni Jenerali katika makao makuu ya Jeshi la Ulinzi la Uganda (UPDF) mjini Mbuya, kusini mashariki mwa Kampala.
Muhoozi Kainerugaba (katikati) akivalishwa cheo kipya cha Luteni Jenerali katika makao makuu ya Jeshi la Ulinzi la Uganda (UPDF) mjini Mbuya, kusini mashariki mwa Kampala.Picha: Joseph Kiggundu/Photoshot/picture alliance

Muhoozi Kainerugaba anachukua nafasi ya Jenerali Wilson Mbasu Mbadi ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa biashara katika mabadiliko mapya ya baraza la mawaziri yaliyotangazwa jana jioni.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi, washauri wake wawili wa karibu pia wamepewa nyadhifa za uwaziri na kuchochea uvumi kwamba Rais Museveni anaunga mkono shughuli za kisiasa Muhoozi Kainerugaba.

Soma pia:  Vuguvugu la MK la Uganda lajigeuza asasi ya kiraia

Mtoto huyo wa kwanza wa rais amekuwa akifanya mikutano ya hadhara kote nchini, hatua ambayo inakwenda kinyume na sheria inayowazuia maafisa wa jeshi kujihusisha na siasa.

Kainerugaba hata hivyo amejitetea kwa kueleza kuwa shughuli zake - ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa hivi karibuni wa kundi la uanaharakati la Patriotic League of Uganda - aliyesema kundi hilo linanuia kuhimiza kujenga uzalendo miongoni mwa Waganda.

Adui wa Museveni ni Museveni mwenyewe - Bobi Wine

Museveni ambaye kwa mara ya kwanza alichukua madaraka kwa nguvu mnamo mwaka 1986, na kuchaguliwa mara sita, hajaeleza ni lini atakapostaafu.

Kiongozi huyo pia hana mpinzani ndani ya chama tawala cha NRM huku wengi wakiamini kuwa jeshi litakuwa na sauti katika kuchagua mrithi wake.

Kulingana na wachambuzi, washirika wa Kainerugaba wameteuliwa kimkakati kwenye nafasi za juu za idara ya usalama. Uganda itaanda uchaguzi mkuu ujao mwaka 2026.