1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

John Pombe Magufuli

John Pombe Joseph Magufuli ndiye rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alichaguliwa Oktoba 2015 na kurithi mikoba ya Jakaya Mrisho Kikwete. Ni mwanasiasa mwenye sifa ya uchapakazi na asiye na mazaha.

Magufuli au JPM kama anavyofahamika, alichaguliwa kwa mara ya kwanza 1995 katika nafasi ya ubunge, na akahudumu katika baraza la mawaziri katika nafasi ya naibu waziri wa ujenzi kuanzia 1995 hadi 2000, waziri wa ujenzi kuanzia 2000 hadi 2006, waziri wa ardhi na maendeleo ya makaazi mwaka 2006 hadi 2008, na waziri wa ujenzi kwa mara ya pili kuanzia 2010 hadi 2015. Akisimama kama mgombea wa chama tawala - Chama cha Mapinduzi CCM, alishinda uchaguzi wa 2015 na aliapishwa Novemba 5, 2015.

Onesha makala zaidi