1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Vivutio vya Utalii

Kila taifa na kila mji unavyo vivutio vyake. Vivutio vya utalii ndiyo hulifanya eneo kuwa maarufu. Vinaweza kuwa majengo, magofu, wilaya nzima za miji au asilia ya kipekee.

Mnara wa Eifel mjini Paris ndiyo mmoja ya vivutio vinavyotembelewa zaidi duniani, lakini hekalu la Angkor Wat nchini Cambodia, Ukuta wa Berlin nchini Ujerumani na Grand Canyon nchini Marekani pia vinastahili kutajwa kama vivutio vikubwa vya utalii duniani. Mara nyingi vivutio vya utalii hugeuka alama zinazofahamika kimataifa na mara zote ni sehemu ya ziara za kitalii. Wakati mwingine vivutio vya utalii vinakuwa vya ajabu kiasi kwamba shirika la UNESCO huvijumlisha kwenye orodha yake ya turaathi za dunia. Huu ni mkusanyiko wa moja kwa moja wa maudhui za DW kuhusu vivutio vya utalii.

Onesha makala zaidi