1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Tanzania

Tanzania ni nchi ya Afrika Mashariki. Inapakana na Kenya, Uganda, Bahari ya Hindi, Msumbiji, Malawi, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Burundi na Rwanda. Ndiyo kubwa zaidi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Jina Tanzania limetokana na Tanganyika na Zanzibar (pamoja na athira ya jina la kale la Azania). Nchi hizo mbili zilikuwa chini ya ukoloni wa Uingereza hadi zilipopata uhuru lakini hazikuwa makoloni ya kawaida. Zanzibar ilikuwa na hali ya nchi lindwa kutokana na mikataba kati ya masultani wa Zanzibar na Ufalme wa Muungano (Uingereza). Tanganyika iliwahi kuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia halafu ikawa chini ya Uingereza kama eneo la kudhaminiwa kutokana na azimio la Shirikisho la Mataifa iliyoweka Tanganyika katika ngazi "B" ya maeneo ya kudhaminiwa. Baada ya kuungana mwaka 1964, ilizaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo mamlaka ya rais wake yanajumlisha hata Zanzibar, ingawa visiwa hivyo vina mamlaka yake ya ndani.

Onesha makala zaidi