1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Uchaguzi Mkuu Kenya 2017

Kenya inajiandaa kwa uchaguzi mkuu Agosti 8, 2017. Wapigakura watamchaguwa rais, naibu wake, wabunge (wawakilishi na maseneta) pamoja na wajumbe wa serikali za ugatuzi (magavana wa kaunti na wawakilishi wa tarafa).

Katiba ya Kenya inataka kuwepo na uchaguzi Jumanne ya pili ya mwezi wa Agosti kila mwaka wa tano. Rais huchaguliwa kupitia mfumo ulioboreshwa wa duru mbili; ili kushinda katika duru ya kwanza, mgombea anapaswa zaidi ya 50% ya kura za jumla na 25% katika kaunti zisizopungua 24. Wabunge 337 wanachaguliwa kwa njia mbili; 290 huchaguliwa katika majimbo. Viti vingine 47 vinatengwa kwa ajili ya wanawake, ambao wanachaguliwa kuwakilisha kaunti 47 za Kenya. Wajumbe 67 wa baraza la Seneti wanachaguliwa kwa njia nne. 47 wanachaguliwa kwa ngazi ya kaunti. Vyama vya siasa vinagawana nafasi 16 za wanawake, mbili za vijana na mbili kwa ajili ya watu wenye ulemavu kulingana na kura jumla vilivyojikingia. Ukurasa huu ni mkusanyiko wa maudhui za karibuni za DW kuhusu uchaguzi wa Kenya 2017.

Onesha makala zaidi