1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaAfrika

Marekani, Kenya kuimarisha ushirikiano wa biashara, uchumi

25 Mei 2024

Marekani na Kenya zitafanya mazungumzo mengine ya biashara mwezi wa sita, wakati mataifa hayo mawili yakipgia debe makubaliano mapya ya biashara na ushirikiano wa kiuchumi kufuatia ziara ya Rais William Ruto Marekani.

https://p.dw.com/p/4gGqM
Marekani | Joe Biden amkaribisha William Ruto
Rais Joe Biden akimkaribisha Rais wa Kenya William Ruto katika Ikulu ya White House mjini Washington, Jumatano Mei 22, 2024.Picha: Susan Walsh/AP Photo/picture alliance

Rais wa Kenya William Ruto alikuwa Washington kwa ziara ya Kiserikali wakati Ikulu ya Marekani ilipoahidi ushirikiano mpya kuhusu teknolojia, usalama na msamaha wa madeni kwa demokrasia hiyo ya Afrika Mashariki.

"Wawekezaji wanapenda kile wanachokiona nchini Kenya," Ruto alisema, akiwavutia viongozi wa biashara kwenye hafla, na kuahidi kurahisisha ufanyaji biashara.

Waziri wa Biashara wa Marekani Gina Raimondo aliwataka viongozi wa biashara kudumisha kasi baada ya matukio ya wiki. "Hatuwezi kwenda nyumbani, kufurahishwa na wikendi na kuendelea," Raimondo alisema. "Sote tuko Afrika, sote nchini Kenya. Twende kufanya mikataba zaidi pamoja."

Marekani | Joe Biden amkaribisha William Ruto
Rais wa Marekani Joe Biden alimkaribisha mwenzake wa Kenya William Ruto katika Ikulu ya Marekani, White House siku ya Alhamisi, Mei 22, 2024 kwa ziara rasmi ya kiserikali.Picha: Susan Walsh/AP Photo/picture alliance

Ofisi ya Mwakilishi wa Biashara wa Marekani ilisema kuwa nchi hizo zitafanya duru ya sita ya mazungumzo ya ana kwa ana chini ya Ubia wa Kimkakati wa Biashara na Uwekezaji (STIP) mjini Mombasa kuanzia Juni 3 hadi 7 baada ya duru ya mjini Washington mwezi huu.

Soma pia: Biden, Ruto waahidi kulinda demokrasia Afrika na kwingineko

Ruto alisema ameshughulikia wasiwasi ulioibuliwa na kampuni ya Google ya Alphabet ili kurahisisha operesheni zake, na kuorodhesha sera kadhaa  za ushuru na nyingine ili kuhimiza uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni.

Google, Miscrosoft zaongoza uwekezaji

Rais wa Alphabet na afisa mkuu wa uwekezaji Ruth Porat alisema Ijumaa kwamba Google inakuza uwekezaji nchini Kenya, ikiwa ni pamoja na katika ushirikiano wa kujenga njia ya kwanza kabisa ya fiber optic kuiunganisha Afrika moja kwa moja na Australia, ambayo inapitia barani humo hadi Afrika Kusini kabla ya kuvuka Bahari ya Hindi hadi Australia.

Ruto aliongeza kuwa Kenya imekuwa ikifanya kazi kuvutia makampuni makubwa ya teknolojia na kampuni changa kupitia "Silicon Savannah" yake na kuongeza kwamba Kenya inalenga katika utengenezaji wa magari ya kielektroniki.

"Serikali ya Kenya katika mfumo ujao wa sera tutakuwa tukiondoa ushuru wote kwa kampuni ambazo zitatengeneza vyombo 100,000 vya kwanza vya magurudumu mawili na magurudumu manne nchini Kenya," Ruto alisema.

Rais wa kampuni ya Alphabet na mkuu wa masuala ya fedha Ruth Porat
Rais wa kampuni ya Alphabet na mkuu wa masuala ya fedha Ruth PoratPicha: Gian Ehrenzeller/EPA-EFE

Shirika la Ufadhili wa Maendeleo ya Kimataifa la Marekani wiki hii lilitangaza mkopo wa moja kwa moja wa dola milioni 10 kwa BasiGo, kampuni ya magari ya umeme inayokodisha na kuuza mabasi ya umeme kwa waendeshaji wa mabasi ya usafiri wa umma nchini Kenya na mkopo wa dola milioni 10 kwa kampuni ya Kenya ya Roam Electric kusaidia utengenezaji wa pikipiki za umeme jijini Nairobi.

Soma pia: Biden, Ruto kujadili msamaha wa deni kwa Kenya wiki hii

Miongoni mwa mikataba iliyotiwa saini siku ya Ijumaa ni pamoja na ushirikiano wa Kenya na Microsoft wa kujenga kituo cha kuhifadhi data cha gigawati 1 chenye thamani ya dola bilioni 1 mjini Naivasha, Kenya ambacho kitatumia huduma za Azure Cloud za kampuni ya Microsoft kwa ajili ya programu zinazotegemea teknolojia ya cloud.

Pikipiki zinazotumia umeme Mombasa Kenya, faida na changamoto ni zipi?

Hatua hiyo itaruhusu serikali ya Kenya kuhamisha data na huduma zake kwa wachuuzi wanaoaminika, ilisema Ikulu.

Rais wa Microsoft Brad Smith alisema chini ya ushirikiano kampuni hiyo itasaidia kuleta huduma za mtandao kwa watu milioni 20 mwaka ujao nchini Kenya.