1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Afrika Mashariki

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inayaleta pamoja mataifa matano ya Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi. Jumuiya hiyo iliasisiwa mwaka 1967, ikavunjika mwaka 1977 na kufufuliwa upya Julai 7, 2000.

Mwaka 2008, baada ya kufanya mazungumzo na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC, na jumuiya ya soko la pamoja la mataifa ya Mashariki na Kusini mwa Afrika COMESA, EAC ilikubali kutanua eneo huru la biashara na kuyajumlisha mataifa wanachama wa jumuiya hizo tatu. EAC ni sehemu muhimu ya jumuiya ya kiuchumi ya Afrika. Jumuiya hiyo inaweka msingi wa shirikisho la Afrika Mashariki, linalotazamiwa kuyaunganisha mataifa yote ya Afrika Mashariki na kuwa taifa moja huru. Eneo la jumuiya hiyo lina ukubwa wa kilomita za mraba 1,820,664 na ina jumla ya wakaazi 149,959,317 (makadirio ya mwaka 2013).

Onesha makala zaidi