Wahamiaji 64 wa Kiafrika wazama nchini Yemen | Habari za Ulimwengu | DW | 23.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Wahamiaji 64 wa Kiafrika wazama nchini Yemen

Wahamiaji 64 wa Kiafrika wamezama katika Ghuba ya Aden wakati wakijaribu kuvuka kutoka Somalia kuingia Yemen .

Miili yao imeopolewa kutoka baharini na wavuvi pamoja na walinzi wa mwambao wa Yemen baada ya mashua ya wahamiaji hao kupinduka nje ya pwani ya jimbo la Chabwa kusini mashariki mwa nchi hiyo.Shirika la habari la serikali nchini Yemen la Saba limesema wahamiaji 25 wasio halali waliweza kukoga hadi ufukweni.

Bado hakuna taarifa juu ya ur aia wao lakini kila mwaka mamia ya Waethiopia na Wasomali wanakufa wakati wakijaribu kuvuka katika safari hiyo ya hatari.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com