Wafuasi watatu wa Bhutto wauwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 08.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Wafuasi watatu wa Bhutto wauwawa

ISLAMABAD

Wafuasi watatu wa Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto wameuawawa kwa kupigwa risasi katika ofisi ya chama chao kusini magharibi mwa Pakistan wakati nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Januari nane.

Washambuliaji walifyatuwa risasi katika ofisi ya chama cha PPP cha Bhuttto kwenye kijiji kilioko mbali katika jimbo la Baluchistan alfajiri ya leo.Katika tukio tafauti mwezi uliopita wafuasi wawili wa chama hicho waliuwawa kwa kupigwa risasi mjini Karachi .

Bhutto hivi sasa yuko Dubai kwa ziara ya kibinafsi kuangalia familia yake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com