Waathirika wa mabomu wasaidiwe | Masuala ya Jamii | DW | 03.09.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Waathirika wa mabomu wasaidiwe

Ripoti ya Shirika moja la kimataifa liitwalo Handicap International lenye makaazi yake mjini Brussles Ubelgiji,iliyotolewa Geneva Uswis imesema kuwa nchi nyingi ambazo zimeuridhia mkataba wa kupiga marufuku mabomu

default

Mtengezaji miguu ya bandia,Freetown

Mkataba huo wa kimataifa ambao, ulianza kutekelezwa March mwaka 1999 umetiwa saini na nchi 156, lakini Marekani, Urusi na China hazijatia saini.Ripoti hiyo imesema kuwa theluthi mbili ya waathirika wa mabomu hayo ya kutegwa ardhini, katika nchi 25, ambao wamepoteza viungo vyao, wanahisi kuwa serikali za nchi zao hazijafanya lolote kuwasaidia.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo la Handcap International, Marc Joolen amesema kuwa haitoshi kwa nchi hizo kuharibu mabomu yaliyoko ardhini na kusafisha ardhi tu,“ Mkataba wa kupiga marufuku mabomu ya ardhini umefanikiwa pale linapokuja suala la kuyaodoa, pamoja na matumizi ya mabomu hayo na milipuko mingine.Hata hivyo kumekuwa na mtizamo mdogo linapokuja suala la waathirika, hawashirikishwi vilivyo katika kutoa maamuzi ya jinsi hali zao zitakavyoweza kubadilika.Hapa suala la kuimarika kwao bado liko nyuma´´,nilazima pia ziwasaidie waathirika wa mabomu hayo ya ardhini,


Kuupigia upatu msaada

Aidha amesema kuwa shirika lake linapigia upatu msaada kwa mamia kwa maelfu ya watu kote duniani waliyoathirika na mabomu hayo ya ardhini pamoja na familia zao kuweza kupatiwa msaada wa kujenga upya maisha yao, na kuongeza kuwa manusura wa mabomu hayo wameachwa katika uwanja mwengine wa mapambano ya kukabiliana na maisha.

Mkurugenzi mtendaji huyo wa Handcap International, amesema kuwa pamoja na kuimarika kwa huduma za kimatibabu kwa waathirika hao, lakini bado wamelazikima kutegemea marafiki au familia zao katika kuendesha maisha yao ya kila siku.

Asilima 70 wa waathirika hawana kazi

Kiwango cha wasio na ajira miongoni mwa watu hao waliyoathirika na mabomu ya ardhini ni kikubwa, ambapo ripoti hiyo imeanisha kuwa kundi hilo limekuwa na nafasi ndogo katika kupata ajira.

Polzisten inspizieren die Stelle wo eine Landmine in die Luft ging

Wakaguzi wa mabomu ya kutegwa ardhini

Ikitolea mfano Stan Brabant ambaye ni mkurugenzi wa masuala ya siasa wa shirika hilo la Handicap International amesema nchini Afghanistan, “Tunaona jinsi watu walioathirika na wanahitaji msaada wa muda mrefu.Muda mwingi tunachokiona ni kwamba msaada mkubwa wamekuwa wakijitafutia wenyewe, au kutoka kwa marafiki, familia au jumuiya.Serikali hazifanyi lolote katika hili.Hii kashfa´´- ambako miongo kadhaa ya vita imekuwa na madhara makubwa, asilimia 70 ya waathirika hao hawana kazi,huku Eritrea ikiwa na karibu asilimia 90 ya wasiyo na ajira.

Firoz Alizada ni kutoka Afghanistan. Alikuwa na umri wa miaka wakati alipokukanyaga bomu lililotegwa ardhini alipokuwa akienda shule na kusababisha kupoteza miguu yake yote miwili.Anasema wao hawahitaji msaada bali ni ajira kama wengine, ´Hatuhitaji msaada, iwapo tutaajiriwa, iwapo tutapewa nafasi ya kufanyakazi hatuhitaji msaada.

Nchi zilizotia saini mkataba huo wa kuzuia mabomu ya ardhini, zinakutana mjini Geneva Uswisi kwa matayarisho ya mkutano mkubwa wa kilele utakaofanyika Disemba mwaka huu huko Cartagena Colombia, kupitia upya mkataba huo.

Susan Eckey ambaye ni mwanadiplomasia kutoka Norway nchi ambayo pamoja na Canada zilikuwa mstari mbele, katika kutiwa saini kwa mkataba huo, amesema mkutano huo wa Colombia unatarajia kuangazia zaidi waathirika wa mabomu hayo ya ardhini.Bibi Susan ndiye atakakyekuwa mweyekiti wa mkutano huo.

Ripoti ya Shirika hilo la Handcap International, imefuatia utafiti uliyofanywa katika nchi 26 ambazo kwa muda mrefu zimekuwa katika vita, ambako majeshi ya serikali au waasi walitumia mabomu hayo ya ardhini na kubakia bila ya kufahamika kwa miaka kadhaa mpaka pale yanapolipuka kwa kuguswa kimakosa.

Mbali ya Afghanistan, nchi nyingine ambazo zimeathiriwa zaidi na mabomu hayo ni pamoja na Angola, Bosnia, Cambodia, Colombia, Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Eritrea, Iraq, Msumbiji, Sudan na Yemen.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/ZPR/REUTERS

Mhariri:M.Abdul-Rahman

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com