VIENNA:Wakaguzi wa IAEA Kuelekea Korea kaskazini baada ya kupata idhini | Habari za Ulimwengu | DW | 11.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VIENNA:Wakaguzi wa IAEA Kuelekea Korea kaskazini baada ya kupata idhini

Wakaguzi wa kimataifa wanajiandaa kwenda Korea kaskazini baada ya nchi hiyo kutoa rasmi idhini ya wakaguzi hao kuingia.

Bodi ya magavana wa shirika la kimataifa la kudhibiti technologia ya Nuklia IAEA imekubali mwaliko huo.

Hii ni mara ya kwanza kwa wakaguzi wa shirika hilo kuingia Korea kaskazini tangu mwaka 2002.

Wakaguzi hao watawajibika kuhakikisha hatua za mwanzo za kuharibu mpango wa kutengeneza sialaha za Nuklia wa Pyongyang.Hatua hiyo inatazamiwa kuwa ngumu na itakayochukua muda mrefu.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com