1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vienna. Katibu mkuu wa zamani wa UM azikwa.

24 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBp0

Katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa na rais wa Austria Kurt Waldheim amezikwa kitaifa jana Jumamosi.

Mamia ya waombolezaji walijikusanya katika eneo muhimu la mjini Vienna la kanisa kuu la Mtakatifu Stefano ili kutoa heshima zao za mwisho za mazishi kwa Waldheim, ambaye muda wake wa madaraka uliingia doa na kugundulika kuhusika kwake na utawala wa NAZI.

Alikiri kuficha ushiriki wake katika jeshi la Hitler katika eneo la Balkan , lakini alikana kufahamu uhalifu wa kivita wa Wanazi katika eneo hilo. Alifariki Alhamis iliyopita kwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka 88.