Utafiti wa kimazingira kabla Copenhagen | Masuala ya Jamii | DW | 04.12.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Utafiti wa kimazingira kabla Copenhagen

Je, dawa mjarabu imegunduliwa kupambana na moshi (Co2 ?)

default

Nembo ya Umoja wa Mataifa kuhusu mkutano wa hali ya hewa mjini Kopenhagen

Katika vita vya kupambana na moshi wa gesi inayochafua hali ya hewa,wataalamu wa utafiti wa kisayansi ,wanatumai wameshagundua silaha mjarabu yenye nguvu mara 3 za kuzuwia uchafuzi huo.

Katika vinu vya bio, (vya kimazingira) inapangwa kuuchuja moshi kutoka hewani na wakati huo huo, vinu hivyo, vizalishe nishati ya kimazingira (bio-fuel) na hata zana za ujenzi .

Panatokota uzuri hapo na mvuke unaopanda juu.Katika mabanda ya ya kuoteshea mimea mbali mbali kwenye maabara kuu ya mji wa Jülich,(Ujerumani) , unaning'inia mpira wa plastiki wa aina ya kunyunyizia maji wenye umbo la V uwazi kuona ndani.Mipira hiyo, imefuatana kwa msururu-tena mmoja baada ya mwengine hadi mia moja kwa jumla.

Katika mipira hiyo, kunachururika aina ya matope ya kijani.Ni matope ambayo, siku zijazo pengine, yatatusaidia walimwengu kuepukana na moshi wa (Co2 ) unaochafua mazingira yetu-alao hivyo, ndivyo watafiti wa kisayansi wanavyotumai.

Matope hayo ya kijani , ni aina ya mwani -majani yanayovunwa baharini au pwani) uliota na kutanda kwa ustadi wa kudumu ; na takriban, huota kila sehemu mbali mbali ulimwenguni.Huota katika chemchem za joto,katika maji mwani huo ,anadai Kostas Schinarakis , mtaalamu wa elimu ya viumbe na mazingira katika maabara hiyo , Isitoshe, una manufaa makubwa ya kula moshi huo wa Co2,kwani, inaupenda ladha yake.

Kostas Schiranakis, Biologe am Forschungszentrum Jülich zwischen den Algen-Kunststoffschläuchen

Kostas Schiranakis, Mtaalamu wa Biolojia akiwa kwenye kituo cha utafiti katika mji wa Jülich, Ujerumani

"Mwani huu wa baharini , ni wa aina ya kipekee, ambao una nguvu na uwezo wa kupambana na moshi huo na kubadili hali ya uchafuzi wa mazingira.Matarajio ni kuweza kuudhibiti moshi huo kwa kiwango kikubwa, mfano , kwenye vinu vya nishati ya makaa ya mawe, na kuchujwa kwa njia ambayo, haupenyi na kupaa hewani."-asema Schinarakis.

Mwani unahitaji kama mimea yote , mwangaza na moshi-hivyo ni kusema , moshi wa (Co2 ) ili ukue.Lakini, ukilinganisha na mimea inayoota aridhini,mwani huota mara 7 hadi 10 haraka zaidi na humeza moshi huo unaochafua mazingira.Mwani wa kiasi cha kilo 2,kwa muujibu wa mtaalamu huyo wa mazingira,humeza kilogramu 4 za moshi huo.

Je, kwa msaada wa mwani , yawezekana kupambana na moshi unaotochafulia mazingira yetu ?

Mtaalamu wa biolojia Schinarakis wa maabara ya Jülich, anasema kwamba, ili kuifikia shabaha hiyo, kutahitajika mamilioni ya fedha ili vinu vya nishati nchini Ujerumani , viweze kuepusha kutoa moshi huo unaotuchafulia mazingira.

Mtayarishi: Ramadhan Ali

Mhariri: Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com