Umoja wa Ulaya waupongeza mpango wa Ugiriki
4 Machi 2010Matangazo
Umoja wa Ulaya umepongeza mpango wa Ugiriki wa kupunguza matumizi ya fedha ya euro bilioni 4.8 ili kujaribu kupunguza nakisi kubwa ya bajeti yake na kupata hakikisho la kusaidiwa kifedha na mataifa ya Ulaya. Mpango huo unajumuisha kupunguza gharama za sekta ya umma, kusitisha malipo ya uzeeni na kuongeza kodi.
Kamishna mpya wa masuala ya nishati wa Umoja wa Ulaya, Guenther Oettinger ameonyesha uwezekano wa umoja huo kuisaidia Ugiriki, lakini amesema nchi hiyo lazima itekeleze jukumu lake kwanza. Ugiriki imesema italigeukia Shirika la Kimataifa la Fedha-IMF kama Umoja wa Ulaya utashindwa kuisaidia.