Umoja wa Ulaya waunga mkono mchakato wa demokrasia
5 Februari 2011Matangazo
Merkel, alitamka hayo alipohotubia mkutano wa usalama wa kimataifa mjini Munich, kusini mwa Ujerumani. Amesema umma wa Misri unaungwa mkono na ameonya kutochukuliwa hatua za haraka. Akaongezea kuwa utaratibu wa kidemokrasia unapaswa kufanyika kwa amani na busara.
Merkel alisema kuwa Umoja wa Ulaya, hapo jana kwa pamoja, uliamua kuwa unataka ushirikiano mpya ili kusaidia kuleta mageuzi hayo kama majirani wao katika mwambao wa Afrika ya Kaskazini.
Wakati huo huo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton alipozungumza kwenye mkutano huo mjini Munich, alitoa mwito wa kufanyika mageuzi halisi ya demokrasia katika kanda hiyo, kufuatia machafuko ya nchini Misri.