Umoja wa Mataifa wamtambua Ouattara. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 09.12.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Umoja wa Mataifa wamtambua Ouattara.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeonya kwamba liko tayari kuweka vikwazo dhidi ya mtu yoyote ambaye atajaribu kuvuruga mchakato wa amani nchini Cote d'Ivoire.

default

Kiongozi wa upinzani nchini Cote d'Ivoire Alassane Ouattara.

Aidha baraza hilo pia limetoa wito wa pande zote kuheshimu ushindi alioupata kiongozi wa upinzani nchini humo Alassane Ouattara, kufuatia uchaguzi wa rais uliofanyika nchini humo mwezi uliopita.

Katika taarifa iliyosomwa na balozi Brooke Anderrson, ambaye nchi yake kwa sasa ndiyo inashikilia nafasi ya Urais, baraza hilo limesema linalaani juhudi zozote zitakazovuruga matakwa ya watu ama kuhujumu uaminifu wa zoezi hilo la uchaguzi.

Rais aliyemaliza muda wake Laurent Gbagbo amekuwa akikataa mpaka sasa kukabidhi madaraka kwa mpinzani wake Alassane Ouattara, ambaye ameshinda katika uchaguzi huo wa Rais.

Elfenbeinküste Wahl Laurent Gbagbo

Rais anayemaliza muda wake Laurent Gbagbo.

Urusi imekuwa ikikawiza jaribio la baraza hilo la usalama kumlazimisha Bwana Gbagbo kuondoka madarakani.

 • Tarehe 09.12.2010
 • Mwandishi Halima Nyanza
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/QTrU
 • Tarehe 09.12.2010
 • Mwandishi Halima Nyanza
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/QTrU

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com