Ukanda wa video waonyesha mateka wa Kingereza | Habari za Ulimwengu | DW | 27.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ukanda wa video waonyesha mateka wa Kingereza

DUBAI:

Kituo cha televisheni cha Al-Arabiya kimetangaza kanda ya video ikimuonyesha mateka wa Kingereza Peter Moore alietekwa nyara nchini Irak mwezi wa Mei mwaka jana.Moore,aliekuwa akiifanyia kazi kampuni ya ushauri ya Kimarekani nchini Irak,alitekwa nyara pamoja na walinzi wake wanne wa Kingereza, walipokwenda katika wizara ya fedha ya Iraq mjini Baghdad.

Inaaminiwa kuwa Waingereza hao walitekwa nyara na kundi la Kishia.Wateka nyara wanataka Wairaki tisa waliozuiliwa jela waachiliwe huru kubadilishana na hao Waingereza watano.Serikali ya Uingereza imeshutumu kutangazwa kwa kanda hiyo ya video ambayo Al-Arabiya imesema imetumwa na kundi moja la Kishia.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com