Ujumbe wa China ziarani Darfur | Habari za Ulimwengu | DW | 08.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ujumbe wa China ziarani Darfur

Beijing:

Ujumbe wa serikali ya China umezitembelea kambi za wakimbizi wa Darfour na kuonana pia na viongozi wa kimkoa.Lengo ni kujionea hali namna ilivyo katika jimbo hilo linalogubikwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2003.Habari hizo zimetangazwa na vyombo vya habari vya China hii leo.Ujumbe wa China ukiongozwa na muakilishi wa serikali ZHAI JUAN umeitembelea kambi ya Abou Chouk-Darfour ya kaskazini na kuzungumza na diwani Youssef Kibir.Ujumbe huo wa China unafanya ziara ya siku nne huko Darfou ambapo unapanga pia kuzitembelea kambi zas Nyala-kusini mwa Darfour wanakokutikana zaidi ya wakimbizi 14 elfu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com