Ufunguzi wa olimpik 08-08-08 | Matukio ya Kisiasa | DW | 08.08.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Ufunguzi wa olimpik 08-08-08

Michezo ya olimpik yafunguliwa Beijing leo tarehe 8:8:8

default

Watibeti waandamana dhidi ya China,India.

Leo ni tarehe 8,mwezi wa 8,mwaka 2008-siku iliochaguliwa na China kuifungua rasmi michezo ya 29 ya Olimpik ya Beijing:

(8) ni tarakimu inayokuletea bahati kwa jinsi wanavyoamini wachina.Ni hivyo, licha ya kuwa Chama-tawala cha kikominist hakiamini itikadi kama hizo. Tarehe hii ya 8-8 jinsi ilivyofuatana uzuri na bahati hiyo,uongozi wa China haukuweza kuepuka kuichagua kuwa ni siku ya kuifungua rasmi michezo ya 29 ya kisasa ya Olimpik katika Uwanja mkuu wa olimpik wa mfumo wa jumba la ndege jijini Beijing.Swali ni je, michezo hii ya olimpik itailetea kweli china bahati njema ?

China ingelihiyari sana kuiandaa michezo hii ya olimpik tangu mwaka 2000.Lakini kutokana na kukandamiza kwake kwa mkono wa chuma na kumwaya damu kukandamiza wimbi la demokrasia nchini hapo 1989,Halmashauri kuu ya olimpik ulimwenguni (IOC) iliamua hapo 1993 kuuchagua mji wa Sydney,Australia,mpinzani wa Beijing wakati ule kuandaa michezo ya mwaka ule.

Mwaka 2001, Beijing ikatamba na kushinda kuandaa michezo inayoanza leo.Ilikua kama mapinduzi kwa chama-tawala cha kikoministi.Kwani, kwa jicho la kinadharia,kiliweza kuwachangamsha wananchi wa China kwa kipindi cha miaka 7 kujiandaa na kuikodolea macho siku ya leo na kujivunia.Kwa jicho hili tangu mwanzo ilikua unafiki dhahiri kudai "kutenganisha spoti na siasa".

Michezo hii ya Beijing ,imelengwa zaidi ndani ya China ili kuanika hadharani kuibuka China dola kuu kwa njia za picha zitazooneshwa n'gambo.

TV ya China, itamuonesha kutoka kila pembe jinsi Rais wa China Hu Jintao anavyochanganyika na marais George Bush,Nicholas Sarkozy au hata waziri mkuu wa Russia, Wladmir Putin.

Risala hapa ni wazi:" Sasa tupo herimu moja na hawa." Kuwa Rais George Bush hapo kabla alikosoa kukiukwa kwa haki za binadamu nchini China , hakuna mtazamaji wa TV nchini China alielezwa au kuoneshwa hayo.Na usiolisikia, hulijui.

Ikisimuliwa kwa mapana na marefu miaka iliopita jinsi michezo ya olimpik ya Korea ya Kusini (1988) -miaka kiasi ya 20 iliopita ilivyoibadili Korea ya Kusini.Lakini, Korea huwezi kuilinganisha na China.Korea kusini ni nchi ndogo na kiulinzi na sera za usalama wake inaegemea Marekani.China ni dola kubwa na inajiamulia mambo itakavyo.Kinyume na ahadi zake ilizotoa kabla, Beijing ilipambana vikali na wale wote wenye mawazo tofauti na yake.

Ni wiki moja tu nyuma, serikali ya China ilifungua kjesi dhidi ya wakili wa kike Ni Yulan, ambae kwa miaka mingi akiwatetea wale waliotaifishiwa majumba na mali zao kwa nguvu.Hapo April mkasa huo ukampata yeye binafsi.Nyumba yake ilibomolewa ili kuunawirisha mji kwa ajili ya olimpik.Alipovinjari kuzuwia kubomolewa nyumba yake hiyo,alitiwa nguvuni na yamkini aliteswa.Hata mumewe hakumuona tangu wakati huo.

Uongozi wa China haukustahiki michezo hii ya Olimpik, bali waliostahiki ni umma wa China.Na hii yatia tamaa......kuweza kuibadili China.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com