TRIPOLI : Wanatiba wa kigeni waliteswa Libya | Habari za Ulimwengu | DW | 10.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TRIPOLI : Wanatiba wa kigeni waliteswa Libya

Mwana wa kiume wa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amekiri kwamba wanatiba wa kigeni waliokuwa wamefungwa nchini Libya kwa madai ya kuwaambukiza watoto wa nchi hiyo virusi vya HIV na UKIMWI waliteswa wakati walipokuwa wakishikiliwa.

Seif al –Islam Gaddafi amekiambia kituo cha televisheni cha Kiarabu cha Al Jazeera kwamba waauguzi hao watano wa Kibulgaria na daktari mmoja wa Kipalestina waliteswa kwa kurushwa na umeme na kutishwa kwa kuambiwa kwamba familia zao zitaandamwa.

Wanatiba hao sita waliachiliwa mwezi uliopita baada ya kusota gerezani kwa miaka minane nchini Libya wote wamesema kwamba walilazimishwa kukiri kuwa na hatia kwa kuteswa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com