1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tokyo.Chama tawala chashindwa kupata wingi wa kutosha.

30 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdq

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema kuwa anapanga kubaki madarakani licha ya kushindwa vibaya katika uchaguzi mkuu wa bunge.

Kulikuwa na uvumi kuwa Abe atajiuzulu baada ya matokeo ya awali kuonyesha kuwa chama tawala cha Liberal Democratic kitapoteza wingi wake katika bunge la nchi hiyo.

Muungano wa vyama vinavyounda serikali unaweza kubaki madarakani kwa msingi wa wingi wa wabunge katika baraza la wawakilishi katika bunge la nchi hiyo .

Huu ni mtihani wa kwanza katika uchaguzi kwa Abe tangu kuingia madarakani miezi 10 iliyopita. Viwango vya maoni ya wapigakura kwa Abe vimeshuka tangu wakati huo, kutokana na kashfa kadha zilizoiandama serikali.