TOKYO;Ajiuzulu kwa kuunga mkono Japan kupigwa bomu la atomik | Habari za Ulimwengu | DW | 03.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TOKYO;Ajiuzulu kwa kuunga mkono Japan kupigwa bomu la atomik

Waziri wa Ulinzi wa Japan Fumio Kyuma amejiuzulu kufuatia matamshi yake ya kwamba shambulizi la bomu la atomik la Marekani nchini Japan, lilikuwa ni njia ya lazima kumaliza vita kuu ya pili ya dunia.

Fumio aliwaambia waandishi wa habari mjini Tokyo ya kwamba Waziri Mkuu Shinzo Abe amekubalia kujiuzulu kwake.

Fumio hapo siku ya jumamosi aliibua ghadhabu miongoni mwa wajapan aliposema kuwa shambulizi hilo la Marekani nchini Japan lisingeweza kuepukika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com