TEHRAN: Wanaharakati wa kike wamekamatwa nchini Iran
5 Machi 2007Matangazo
Zaidi ya wanaharakati 30 wa kike wamekamatwa katika mji mkuu wa Iran Tehran.Wanawake hao walikusanyika nje ya mahakama mjini Tehran, kuwaunga mkono wenzao 5 wanaopigania haki za wanawake.Wanawake hao 5 wamefikishwa mahakamani kwa sababu mwaka jana waliandaa maandamano kupinga sheria ambazo wamesema huwabagua kijinsia.Wanaharakati hao wameshtakiwa kuhatarisha usalama wa taifa na kushiriki katika maandamano yasio halali.